Wabunge wa Jubilee watakiwa kuidhinsha miswada bila mabadiliko

Bunge la kitaifa linaendelea kujadili mswada wa kuzifanyia mabadiliko sheria za uchaguzi, unaolenga kufanikisha maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Hata hivyo, nipe nikupe imesheheni kati ya wabunge wanaounga mkono pendekezo la kuharamisha mtindo wa wanasiasa kuhamahama vyama baada ya chaguzi za mchujo, na wale wanaopinga pendekezo hilo. Francis gachuri ana vidokezo vya mjadala huo.