Viongozi wa Jubilee wakita kambi Embu

Rhumba la Jubilee hii leo lilisakatwa katika kaunti ya Embu, pale ambapo suala la ufisadi lilipewa kipau mbele huku Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wakiwasuta viongozi wa upinzani kwa kile walikitaja kama kutumia  fedha zilizopatikana kupitia sakata za ufisadi kufadhili kampeni zao.