Tobiko aagiza maafisa 7 wa benki ya Family washtakiwe

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma keriako tobiko ameamrisha maafisa saba wa benki ya family akiwemo aliyekuwa afisa mkuu peter munyiri washtakiwe kwa makosa yanayohusiana na sakata ya wizi wa milioni 791 za huduma ya nys.

Munyiri na maafisa wenza watashtakiwa kwa makosa ya kutozingatia kanuni za benki pamoja na kuwezesha ulanguzi wa pesa. Haya yanajiri huku mahakama ikitoa nafasi kwa aliyekuwa naibu mkurugenzi mkuu wa nys aden harakhe na afisa wa wizara ya ugatuzi hassan noor washtakiwe kuhusiana na sakata hiyo.