Shehena ya karatasi za kura yawasili Nairobi kutoka Dubai

Mahakama ya Rufaa hapo kesho itatoa uamuzi iwapo tume ya Uchaguzi IEBC itaruhusiwa kuendelea kuchapisha karatasi za kura ya urais katika kampuni ya Al Ghurair huko Dubai au watalazimika kutoa kandarasi hiyo upya.
Hii ni katika rufaa iliyowasilishwa na IEBC wiki iliopita, uamuzi wa mahakama hiyo ukiwa na uwezo wa kuathiri kalenda ya uchaguzi endapo IEBC itashindwa.
Haya yanajiri huku tume hiyo ikipokea karatasi za kupigia kura za ugavana katika kaunti 41.
Karatasi za kaunti sita zikiwemo Nyeri, Nairobi, Siaya, Mombasa na Baringo zingali kufika baadhi yake kutokana na kesi ambazo zilichelewesha kuanzwa kwa uchapishaji.