Rais atoa hakikisho kuwa mchujo wa Jubilee utakuwa huru

Rais Uhuru Kenyatta ameendelea kuwahakikishia wanasiasa chini ya mrengo wa Jubilee kwamba kila mmoja atapewa nafasi kuwania nafasi yake kupitia kura uya mchujo bila mapendeleo. Akiwa katika ziara ya eneo la Pwani, Rais amewashawishi wanajubilee ambao wiki ijayo wanatarajiwa kujiunga na chama kipya cha Jubilee kutohofia uanasiasa wao. Haya yanajiri siku moja tu baada ya bunge la kitaifa kupitisha mswaada unaoharamisha kuhama kwa wanachama katika chama cha kisisasa endapo watapoteza tikiti ya chama kabla ya uchaguzi.