Mtangazaji mkongwe wa Ramogi FM azikwa

Mtangazaji mashuhuri wa Ramogi Fm Patrobas Agao aliyefariki wiki tatu zilizopita amezikwa leo katika eneo bunge la Nyakach Kaunti ya Kisumu katika hafla iliyohudhuriwa na familia, wafanyikazi wenza na maelfu ya mashabiki wake. Agao amekumbukwa kama kielelezo chema kwa jamii haswa kwa nyanja yake ya uanahabari ambapo amewakuza vijana wengi kuwa wanahabari bora. Mwanahabari wetu Gatete Njoroge ametuandalia taarifa hiyo