Mama Nzisa asherehekea miaka 100

Familia, jamaa na marafiki wa Mama Lusia Kamitu walipata fursa ya kipekee hapo jana kuadhimisha miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Mama Kamitu ambaye alizaliwa mwaka wa 1917. Sherehe hiyo maalum iliyofanyika katika eneo la Matungulu kaunti ya Machakos ikiwa fursa bora ya kuwaleta pamoja familia yake na jamii kwa jumla.