Maafisa wa EACC wachunguza madai ya ufisadi kaunti ya Kilifi

Wabunge kutoka kaunti ya kilifi sasa wanamtaka gavana wa Kilifi Amason Kingi  awasimamishe  kazi mawaziri wanaotuhumiwa kwa ufujaji wa mamilioni ya pesa za kaunti hiyo.

Wabunge hao pia wameihimiza tume ya kupambana na ufisadi nchini eacc kurakakisha na kukamilisha uchunguzi wa sakata hiyo ya zaidi ya shillingi milioni hamsini kama anavyotueleza mwanahabari wetu  Stephen Letoo.