Kizungumkuti cha mahindi: Waziri Kiunjuri ahojiwa na Seneti

Kizungumkuti cha mahindi: Waziri Kiunjuri ahojiwa na Seneti

Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri leo amehojiwa na kamati maalum ya bunge la seneti inayochunguza utata wa malipo ya mahindi nchini.

Kiunjuri ametakiwa kueleza utata unaogubika malipo hayo ambapo amewaambia maseneta kuwa serikali tayari imelipa shilingi bilioni 9.4 kwa zaidi ya tani milioni tatu za mahindi wakati wa msimu wa mwaka wa 2017/2018.

Waziri pia ametakiwa kutoa hakikisho kuwa Kenya kuna usalama wa chakula.