Kamati ya bunge yamhoji wakili wa seneta Murkomen

Wakili wa kampuni ya Sing’oei, Murkomen and Sigei, inayohusishwa na seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen amekanusha kupokea fedha zozote zinazohusiana na sakata ya NYS. Katika mahojiano na kamati ya bunge kuhusu uhasibu, Sigei amesema kuwa uhusiano wake na kampuni ya “Out the Box” ulikuwa wa wakili na mteja na ulihusu pesa za kununua ardhi wala si miradi ya NYS.