Kalonzo akanusha madai kwamba ataihama NASA

Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka amekanusha madai ya kuwa na njama ya kung’atuka NASA, lakini akamtetea kinara wa wachache katika bunge la kitaifa Francis Nyenze dhidi ya matamshi aliyotoa juzi kuhusiana na hali ilivyo katika muungano wa upinzani. Musyoka amesisitiza yuko ndani ya NASA hadi mwisho, lakini akataka semi za wale wanaounga mkono azma yake ya urais ziheshimiwe, sawa na zile za wafuasi wa vinara wenza wa NASA.