Juhudi za kurejesha usalama bonde la ufa

Huku visa vya ukosefu wa usalama vikiendelea kuwa donda ndugu baina ya jamii za wapokot na waturkana, wachambuzi wanawanyooshea kidole cha lawama baadhi ya viongozi wa jamii hizo ambao wanadai hunufaika kutokana na wizi wa mifugo; jambo linalosababisha jamii mbili hizo kuhasimiana mara kwa mara.