Jeshi lachukua mamlaka ya utawala jijini Harare

Hali si hali nchini Zimbabwe baada ya wanajeshi kuchukua hatamu za uongozi wa nchi hiyo siku moja tu baada ya mkuu wa wanajeshi kutangaza kuwa hawataruhusu viongozi waliopigania uongozi wa taifa hilo kunyanyaswa na maafisa wachache wa chama tawala cha ZANU-PF. Haya yanajiri siku chache baada ya makamu wa rais Emmerson Mnangagwa kufutwa kazi kwa madai ya kutaka kumwondoa mamlakani Rais Robert Mugabe.