Inadaiwa kuwa Ksh. 45 milioni zimefujwa kaunti ya Kilifi

Siku kadhaa baada ya kuripotiwa kupotea kwa takriban shilingi milioni 45 kutoka kaunti ya Kilifi, gavana Amason Kingi amewaachisha kazi maafisa kumi ambao wanashukiwa huenda walihusika kwenye sakata hii huku uchunguzi ukifanyika.