Hatua ya Bahati kukalia kiti cha rais yaibua hisia mseto

Kuzinduliwa rasmi kwa chama cha Jubilee hapo jana kuliambatana na mbwembwe  na madoido ya aina yake lakini kile ambacho kimesalia vinywani mwa wakenya wengi ni tumbuizo la mwanamuziki wa nyimbo za injili Kevin Bahati almaarufu ‘Bahati’. Hatua yake ya kumwondoa Rais Uhuru Kenyatta kwenye kiti chake na kukalia kisha  kumwimbia mama wa taifa Margaret Kenyatta pamoja na kuweka mguu wake juu ya meza ya naibu rais William Ruto imezua hisia mseto huku wengi wakilalamika kuwa alivuka mipaka.