Gladwel Wairimu hutunza maiti Voi

Katika ulimwengu wa sasa ambapo ajira zimekuwa adimu, kila mmoja hufanya bidii masomoni angalau kuajiriwa ili kuyakithi maisha yake. Katika mji wa Voi kaunti ya Taita Taveta mwanamke mmoja kwa jina Gladwel Wairimu ameshangaza wengi baada ya kuajiriwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, kazi ambayo watu wengi huiogopa.