Gharama ya amani kati ya Samburu na Pokot

Wafugaji kutoka jamii ya Wasamburu wanaoishi katika maeneo yaliyo karibu na mipaka ya kaunti ya Samburu na Baringo wamedhamiria kudumisha amani kati yao na jamii jirani ya Wapokot. Jamii hizo zimekuwa zikikabiliana katika uvamizi wa kulipiza kisasi cha wizi wa mifugo. Lakini sasa wameapa kusahau yaliyopita na kuboresha uhusiano mwema ili kujenga taifa na mustakabali wa vizazi vyao.