69% ya Wakenya wataka wakimbizi warudi makwao

Asilimia sabini ya wakenya wanahisi kuwa serikali inafaa kuwaondoa wanajeshi wa kdf nchini Somalia.

Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa kampuni ya twaweza East Africa unaobaini kuwa asilimia 53 ya wananchi wanapendekeza kuwa wanajeshi hao wanafaa kurejea hadi mipakani kulinda taifa hili dhidi ya magaidi.

Wakati uo huo utafiti mwingine wa Ipsos umebaini kuwa Wakenya wengi wanahoji kuwa kuendelea kuwa kwa kdf nchini somalia ndio chanzo cha mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya.