Wabunge wajadili kipengee cha kuhamahama vyama

Bunge la kitaifa limeikarabati ripoti ya kamati teule, na kukiondoa kipengee kilichokusudia kuharamisha mtindo wa wanasiasa kuhamahama vyama. Hata hivyo, kuidhinishwa kwa mabadiliko hayo yaliyopendekezwa na mbunge wa kisumu mjini Magharibi Olago Aluoch yalipingwa na kiongozi wa wengi Aden Duale, aliyekosoa utaratibu uliofuatwa. Na huku wabunge wengi wakipigia debe wazo la Aluoch, naibu spika Dkt. Joyce Laboso aliahirisha kikao, ili kutoa nafasi ya mashauriano kati ya wabunge na vinara wa miungano ya jubilee na Cord kuhusu hatma ya ripoti ya kamati teule. Bunge la seneti hata hivyo liliidhinisha ripoti hiyo bila mabadiliko yoyote

latest stories